Bingwa wa taji la Afcon mwaka 2021 mwite Sadio Mane atakosekana katika mechi ya leo ya klabu bingwa ulaya ambapo kikosi cha Bayern Munich Kitasafiri kwenda jijini Paris Ufaransa kuvaana na PSG.
Sadio Mane amekuwa mkekani kwa kipindi cha miezi mitatu sasa baada ya kupata jeraha mwaka jana katika mechi za Bundesliga, jeraha ambalo lilimkosesha nafasi ya kuungana na wachazaji wenzake wa Simba wa Teranga (Lions of Teranga) katika mashindano ya kombe la dunia mwezi Disemba.
Wachezaji wengine watakao kosekana katika mechi ya ugenini kwa upande wa Bayern Munich ambao ni miamba ligi kuu ya Ujerumani ni pamoja na Manuel Neuer ambaye alivunjika mguu mwezi Disemba pamoja na Lucas Hernandes raia wa Ufaransa.

