WATALII ZAIDI YA ELFU MOJA WAMEWASILI KATIKA BANDARI YA MOMBASA

Meli ya watalii zaidi ya elfu moja imewasili nchini na kutia nanga katika bandari ya mombasa.
Meli hiyo kwa jina MV. Atania imewaleta watalii hao kutoka mataifa ya Madagascar na Mauritius, watalii ambao baadaye wanatarajia kuondoka hadi Zanzibar kabla ya kurejea makwao.
Mamlaka ya bandari nchini KPA imesema kuwa serikali kupitia wizara husika itaboresha sekta ya utalii kwa minajili ya kuongeza mapato ya kitaifa.