Kati ya wakenya takribani milioni 1.5 wanaougua ugonjwa wa kifafa kote nchini, elfu 14 kati ya wakenya hao ni wakaazi wa kaunti ya Kilifi.
Haya ni kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya Kifafa kaunti ya Kilifi Daktari Eddy Chengo, ambaye amesema kutokana na kuwepo kwa idadi hiyo, ipo haja ya mashirika ya kijamii, Serikali ya kitaifa pamoja na ile ya kaunti ya Kilifi, kushirikiana katika kuweka jitihada zaidi za kukabiliana na ugonjwa huo kaunti hii ya Kilifi.
Kauli yake imeungwa mkono na mwenyekiti wa watu wenye uatilifu wadi wa Kakuyuni kaunti ya Kilifi, Thomas Mwakombe na kasisi wa kanisa la kianglikana mjini Malindi, Samuel Jeffa Yaa ambao wamesema kuwa sherehe hizo zinapaswa kufanyika mjini Kilifi, karibu na afisi za serikali ya kaunti, ili kusaidia kuhamasisha walengwa na jamii kwa jumla kuhusiana na maradhi hayo.
Aidha, baadhi ya wazazi wa watoto walio pona na baadhi ya wale ambao bado wanaugua maradhi hayo, wakiongozwa na Francis Kalu pamoja na Perris Haluwa, wameionya jamii dhidi ya kutengemea wanganga na waombezi na badala yake kufika hospitalini ili kupata ushauri wa daktari.
Jana ulimwengu uliadhimisha siku ya kifafa duniani.
WATU ELFU NNE WANAUGUA KIFAFA KAUNTI YA KILIFI

