Mkufunzi wa klabu ya Malindi Progressive Elly Katana anasema kwamba kwa sasa wanazingatia kutia jitihada hata zaidi ili kuona wanaandikisha matokeo mazuri katika mechi ijyo baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Rainbow katika uwanja wao wa nyumbani Alaskan ulioko kaunti ya kilifi.
Mkufunzi Katana amesema bado kuna matumaini ya kumaliza vizuri msimu huu kwani katika ligi hiyo ya daraja la kwanza hakuna mapengo makubwa tofauti na aliyeko nafasi ya kwanza Young Bulls na nafasi ya pili Nairobi United ambako kwa sasa kuna utofauti wa alama 12.
Kuondokewa na wachezaji ndio tatizo kuu linalomponza mkufunzi Elly kwa sasa kwani ako na nafasi sita za kikosi cha kwanza anazofaa kujaza ili kuimarisha kikosi chake.

