MALINDI PROGRESSIVE YAKAUKIWA NA USHINDI MECHI NNE MFULULIZO

Klabu ya Rainbow FC kutoka kaunti ya Nairobi imesajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Malindi Progrrssve katika uwanja wa Alaskan mechi ambayo imetamatika muda mfupi uliopita.

Akizungumza baada ya mechi hiyo mkufunzi wa Rainbow fc Fred Mwaile amesema kwamba amefurahishwa na matokeo ya mechi hiyo ugenini licha ya mchezaji wake mmoja kupigwa kadi nyekundu na amesema kwamba matokeo hayo yanazidi kuchochea moto wa kupanda daraja la National Super League.

Kwa upande wake mkufunzi wa Malindi Progressive Elly Katana ameeleza kusikitika kwa matokeo hayo akisema kwamba wamepoteza nafasi nyingi ambazo wameshindwa kuzalisha mabao.

Hata hivyo Katana amesema kwamba kuondokewa na wachezaji takriban sita ambao hucheza katika kikosi cha kwanza ndio jambo linaloponza klabu hiyo kwa sasa.Kufukia sasa Malindi Progressive imeshindwa kusajili ushindi katika mechi ya nne mfululizo.

Bernand Lusi ambaye ni nahodha wa Malindi Progressive klabu inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza kitaifa amesema kwamba mbali na baadhi ya wachezaji hao kutorejea kwa wakati, uchovu wa kucheza mechi nyingi ndio jambo ambalo limepelekea kuandikisha matokeo hayo mabaya mpaka kufikia sasa.