John King’oo ambaye ni nahodha wa klabu ya Kamtonga fc kutoka kaunti ya Taita Taveta inayoshiriki ligi ya daraja la pili kitaifa huenda akasalia mkekani kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na jeraha alilopata mwezi machi mwaka huu alipovunjika mguu wake katika mechi dhidi ya klabu ya Yanga kutoka Malindi katika uwanja wa Alaskan ulioko kaunti ya Kilifi.
Akithibitisha hayo mkufunzi wa klabu ya Kamtonga Francis Odemba amesema kwamba kwa sasa Kingoo bado anaendelea na matibabu baada ya kuwa na changamoto ya kupata huduma za matibabu awali ambapo kulikuwa na hitilafu katika kutibiwa mguu huo.
Hata hivyo Kamtonga FC imeanza kupumua baada ya kipindi kirefu cha kuwa na changamoto ya usafiri uliokuwa unawaponza katika misimu iliyopita hasa baada ya kupanda daraja hadi daraja la pili kitaifa.
Kulingana na mkufunzi Odemba ni kwamba serikali ya kaunti hiyo imeingilia kati na kuokoa jahazi kwa kufadhili usafiri wa wachezaji hao

