Waziri wa michezo hapa nchini Ababu Namwamba ametoa wito kwa viongozi wa mashirikisho ya soka katika ngazi tofauti tofauti hapa nchini kutoruhusu vilabu visiyokuwa na timu ya wachezaji wachanga maarufu kama ‘academy’ kushiriki ligi zao kama njia moja ya kuhamasisha umuhimu wa kukuza vipaji katika umri mdogo ambao baadaye watasaidiwa na serikali.
Kama wizara ya michezo Ababu amesema kwamba wanalenga kuandaa kambi za mafunzo kwa wachezaji wachanga katika kila likizo kufunza wachezaji hao wachanga jinsi ya kusakata soka la ushindani baada ya kuteuliwa kutoka mashinani mwa taifa hili la Kenya.
Namwamba alikuwa anayasema hayo wikendi iliyopita katika hafla ya kupeana zawadi kwa wachezaji walioshiriki kwenye mashindano ya Rausha Kipaji mashindano ambayo yalikuwa yanahusisha wachezaji wachanga.

