Waziri wa usalama wa ndani nchini Profesa Kithure Kindiki, ameahidi kuboresha mazingira ya wafungwa katika idara ya magereza humu nchini.
Kulingana na Kindiki ni kuwa serikali, itahakikisha kuwa kila mfungwa anapewa kitanda chake na hata kuboresha baadhi ya vifaa vinavyo tumika katika kuwafunza taaluma mbali mbali.
Akizungumza katika gereza la Embu kaunti ya hiyo ya Embu, waziri kindiki amesema kuwa shughuli ya kuboresha na kuongeza vifaa vya wafungwa kujifunza taaluma mbali mbali, kutagharimu serikali kima cha shilingi bilioni moja.
Wakati uo huo amesema kuwa kama njia mojawapo ya kupunguza idadi ya wafungwa katika magereza, waziri huyo amesema serikali itatumia utaratibu wa msamaha wa rais kwa baadhi ya wafungwa kuachiliwa huru katika magereza hayo.

