WAKUFUNZI WA KENYA WABADILISHANA TABORA UNITED

Siku chache baada ya kufutwa kwa Fransis Kimani kama kocha mkuu wa klabu inayoshiriki ligi ya Tanzania Bara NBC Tabora United, klabu hiyo sasa imempa kazi Brian Aswani kama kocha wa muda.

Aswani ni raia mwengine wa Kenya atakaye iongoza Tabora United kwa muda hadi pale klabu hiyo itakapopata kocha mpya

Aswani ambaye amefanya kazi kama mchamuzi wa soka kwenye televisheni katika mechi yake ya kwanza kama kocha wa Tabora United alisajili ushindi dhidi ya Pamba Jiji Fc.

Kocha huyo ni mmiliki wa cheti cha ukocha chenye kiwango cha Caf B