Huenda timu ya taifa ya soka ya Harambe stars ikaanza kushiriki mechi zake za nyumbani katika viwanja vya Kenya tofauti na mechi kadhaa za awali kutokana na ukarabati wa viwanja unao endelea kwa sasa.
Kipchumba Murkomen akizungumza katika jiji la Nairobi amesema ukarabati huo unafanyika kwa kasi sana haswa katika uwanja wa Nyayo na Kasarani.
Amebainisha kuwa wizara hiyo ilialika Maafisa wa CAF kuja Kenya na kufanya ukaguzi na kupeana mapendekezo yao.
”Kumekuwa na changamoto ya timu za kenya kushiriki mechi zake katika taifa za kigeni, sasa ukarabati wa timu zetu unaendelea kwa kasi na hivi punde timu za kenya zitakuwa zacheza hapa nchini. Uwanja wa Kasarani na Nyayo ndio viwanja ambavyo tumevipa kipaumbele,” Alisema Murkomen
Ikumbukwe kuwa awali Caf kabla ya kuanza kwa ukarabati huu ilitangaza kuwa viwanja ya Nyayo Kasarani havikiwa na hadhi ya kuandaa mechi za kimataifa.

