JUNIOR STARLETS HATIMAYE YASAJILI USHINDI WA KWANZA KWENYE KOMBE LA DUNIA

Kocha wa timu ya taifa ya Harambee Jr Starlets mwite Mildred Cheche anasema amefurahishwa na jinsi wasichana wake walijituma kupatia Kenya ushindi wa kwanza katika ngazi ya Kombe la Dunia.

Akizungumza baada ya ushindi wa alama tatu licha ya kuwa Junior starlets imetmwa katika mashindano hayo kwa kupoteza mechi mbili anasema ipo haja ya wachezaji hao kuwekwa kambini mara kwa mara pamoja na kuhusishwa kwenye mechi ya kimataifa hata kama ni za kirafiki ili kuwapa uzoefu.

Lorna Faith ambaye alichaguliwa kama mchezaji bora katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Mexico usiku wa leo anasema ataishi kukumbuka tuzo ambayo amepewa katika mashindano hayo.

Valerie Nekesa ndio mchezaji wa kwanza wa Kenya kuwahi kufunga katika mashindano ya FIFA ya soka ya Kombe la Dunia ambaye pia ana hili la kusema