WACHEZAJI 39 WATEULIWAKUWAKILISHA KILIFI KATIKA MASHINDANO YA KYISA MWEZI APRILI

Wachezaji 39 kutoka mashinani mwa kaunti ya Kilifi wikendi hii walibahatika kupata nafasi ya kipekee kuteuliwa  kuingia katika kikosi kitakachowakilisha kaunti ya kilifi katika mashinando ya Kenya Youth Inter County Sports kwenye soka na mpira wa wavu yatakayofanyika kaunti ya Tharaka Nithi kuanzia tarehe 23 mwezi huu.

Zoezi hilo lilifanyika katika uwanja wa Mac One ulioko mjini Kilifi siku ya jumamosi na kusimamiwa na Naftali Owino ambaye ni Afisa mkuu wa vijana na michezo kaunti hii pamoja na mwenzake wa biashara na utalii George Mwangiri lakini pia Herbat Mwachiro wa mazingira ambao waliwapa pongezi wachezaji hao.

Vijana hao wenye umri usiozidi miaka 23 wanatarajiwa kukita kambi kuanzia tarehe 16 mwezi huu kwa ajili ya mazoezi watapokuwa wanajitayarisha kwa mashindano hayo ya mwaka huu.