VILABU VIKUBWA ‘EPL’ VYAPIGWA HUKU WAKUFUNZI WAKIFUTWA

Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Graham Potter amefutwa kazi rasmi na klabu hiyo kutokana na muendelezo wa matokeo mabaya katika ligi kuu nchini uingereza. Hatua hiyo ilijiri saa chache baada ya Chelsea kutandikwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Aston Villa.

Mkufunzi huyo ambaye amekaa Chelsea kwa kipindi cha chini ya miezi 7 pekee tofauti na mkataba wake wa miaka 5 ameshinda mechi saba pekee kati ya 22 za ligi kuu nchini uingereza baada ya kuchukua nafasi ya mkufunzi Thomas Tuchel mwaka jana.

Kwa sasa Chelsea inasimama katika nafasi 11 baada ya mechi 28 wakiwa na alama 38.

Katika taarifa nyingine zinazofungamana na kufutwa kazi ni kwamba klabu ya Leicester city pia imemfuta kazi Brendan Rogers kutokana na muendelezo wa matokeo mabaya, hasa baada ya kutandikwa na klabu ya Crystal palace wikendi hii katika ligi ya Primia.

Manchester united jana walipoteza mechi yao ya ligi kuu nchini uingereza dhidi ya Newcastle United katika uwanja wa st James Park.

Bao la Joe Willock mchezaji wa zamani wa Arsenal na lile la Callum Wilson ndio mabao yalotosha kuwapa ushindi Newcastle United.

Kwenye matokeo mengine ni kwamba Westham United walisajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Southhampton.