Beki kigingi Shee Ali ameachana rasmi na klabu ya Young Bulls inayocheza daraja la kwanza kitaifa na kusajiliwa na klabu ya Furunzi FC inayocheza ligi ya daraja la pili kitaifa.
Kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa difenda huyo hajakuwa akipiga zoezi na Young Bulls inayoongoza ligi ya daraja la kwanza kutokana na kukosa nafasi pamoja na muda wa kucheza katika klabu hiyo inayoongozwa na mkufunzi Ali Said Gaucho.
Kwa sasa Shee Ali anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Furunzi katika kipindi hiki huku klabu hiyo inayoongozwa na mkufunzi Nero ikizidi kuwinda wachezaji wengine ili kuipa kasi katika mzunguko wa pili wa msimu huu wa mwaka 2022/2023.
Ikumbukwe kwamba klabu ya Furunzi inalia uhaba wa wachezaji wenye uzoefu kutokana na wachezaji muhimu kuachana na klabu hiyo kwa masuala ya kiuchumi pamoja na wengine ambao ni wanafunzi kurejea masuala ya elimu.

