Wito umetolewa kwa viongozi wa vilabu kuja mashinani na kutambua na kuchukua talanta za wachezaji na kuzitumia katika vikosi vyao.
Ni kauli ambayo imetolewa na meneja wa mauzo katika kampuni ya Dola Sadddam Suleiman ambaye anasema mashindano yanayoendelea ya dola yamevutia watu wengi ambao ni pamoja na wale wanao kuja kusaka talanta.
Amesema itakuwa busara iwapo watachukua wachezaji na kuwa weka katika timu zao.
Ameyasema hayo baada ya kutamatika kwa fainali ya Dola Super Cup kaunti ya Kilifi ambapo Kilifi Kusini iliibuka bingwa siku ya jumapili katika uwanja wa Alaskan. Kilifi South sasa wanasubiri kuingia kwenye mashindano ya kimkoa ambapo bingwa atashinda milioni 1 pesa taslim za Kenya.

