TUTAWAKILISHA KILIFI VYEMA – COACH MANGI

Mkufunzi Abdula Mangi anayesimamia maarufu kama Coach Mangi anayesimamia timu ya Kilifi Kusini kwenye mashindano ya Dola Super Cup anasema yuko na imani kubwa kuwa wataiwakilisha vyema kaunti ya Kilifi katika mashindano hayo.

Mangi Akizungumza na Tama La Spoti anasema mchezo wa Fainali wa jana walioshinda kupitia matuta baada ya tisini kuisha ikiwa sare ya bao 1-1 anasema ulikuwa mchezo rahisi kwake.

Ustadhi Athman Said ambaye ni mwenyekiti wa mashindano ya Dola kaunti ya Kilifi anasema anaimani na kikosi cha Kilifi South kuwa kitafanya vyema Mombasa wanakokwenda kupigania taji la kimkoa ambako mshindi atatuzwa milioni. Hata hivyo anasema mashindano hayo yamekuwa SHWARI KILIFI.