VIONGOZI WA SOKA MASHINANI WAANZISHA MAFUNZO YA MAREFA NA MAKOCHA

Wadau wa soka nchini Kenya wanapozidi kususubiri ligi kurejea kwa hali shwari baada ya swala zima la marufuku ya FIFA kuondolewa na ujio wa waziri mpya wa michezo Ababu Namwamba kuanza rasmi kazi yake, sasa washikadau wa michezo mashinani wameazimia kuanzisha mafunzo ya makocha ili kuboresha sekta hiyo wakati wakisubiri hali nzuri kurejea.

Akizungumza na Tama la Spoti Hamisi Mwakoja ambaye ni mwenyekiti wa soka la kaunti ya kwale amesema kwamba mwishoni mwa mechi huu wa October wataanza rasmi mafunzo ya wakufunzi katika kaunti hiyo ya kwale.

Aidha Hamisi Mwakoja amewaomba washikadau wote mashinani, viongozi wa michezo pamoja na wachezaji kuzidisha mauzo ya soka la kwale ilikuchochea wawekezaji ambao watachangia pakubwa kwenye makuzi ya michezo katika kaunti hiyo.