Bingwa wa Berlin marathon mwite Eliud Kipchoge ameshauri umma hasa wa barani Afrika kulifikiria kwa uzuri suala la kuchangia viungo vya mwili kwa wahitaji ili kuokoa maisha kama wanavyofanya wenzetu Ulaya.
Bingwa huyo wa Olimpiki aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na kituo kimoja cha habari jijini Nairobi ambapo alishauri umma ulimwengu unabadilika na sasa muda umefika tunafaa kujali suala la maisha na ustahimilivu kwa jamii katika bara hili ambapo watu wengi wanaishi na hali tete kiafya.
Ikumbukwe kwamba wiki hii Kipchoge alipata heshima ya kipekee kutoka kwa wadau wa kampuni ya magari ya Japan ya Isuzu, kampuni iliyotangaza kwamba imezindua gari la makala ya ‘Eliud 159’ kuenzi ubingwa wa nguli huyo uliojulikana ulimwenguni kama Ineos 159 maarufu kama ‘No human is Limited.’

