Vilabu vya soka la kinadada katika eneo bunge la Malindi kaunti ya kilifi vinalilia kutelekezwa na viongozi wa eneo hilo, viongozi ambao wamefeli kuwashika mkono katika suala la kuendesha mechi zao.
Neema Charo ambaye ni nahodha wa klabu ya Malindi Progressive starlets akizungumza katika halfa ya kupenwa vifaa vya michezo na mbunge wa Malindi Amina Mnyazi, alitoa wito kwa uongozi wa eneo hilo kuwapiga jeki ili kupata mafanikio viwanjani.
Neema amesema kwamba katika eneo hilo kuna talanta nyingi za kinadada lakini wanakosa motisha kwa changamoto zinazowakabili hasa katika msimu huu.
Nahodha huyo ametoa wito kwa mbunge Mnyazi kuungana na msimamizi wa klabu hiyo ya Malindi Progrrssive Starlets bwana Rashid Odhiambo ili kuwasaidia kinadada hao, akisema kwamba matatizo ya wanawake yanaeleweka vyema na wanawake wenyewe.
Hayo yanajiri baada ya Mbunge Mnyazi mwishoni mwa wiki jana kupiga jeki urekebishwaji wa basi la wachezaji wa Malindi kwa kupeana hundi ya laki moja na elfu sabini kurekebisha basi lililonunuliwa na mbunge wa zamani Aisha Jumwa.
