BILA CAF A HUONGOZI KLABU 2024/2025 – NICK MWENDWA

Rais wa shirikisho la soka hapa nchini Nick Mwendwa, amethibitisha kwamba kuelekea msimu ujao wa mwaka 2024/2025 makocha wote ambao watakuwa wanaongoza vilabu vinavyoshiriki katika ligi kuu ya fkf watafaa kuwa na cheti cha ukocha leseni ya CAF A.

Amezungumza hayo kipindi ambacho FKF imekuwa ikifanya uhamasisho pamoja na mafunzo ya makocha kote nchini ili kuona kwamba makocha wanaelimika ili kusaidia timu za vijana wengi mashinani.

Wiki jana katika kaunti ya Kwale makocha 29 walifuzu na vyeti vya leseni ya CAF D baada ya mafunzo ya siku 10 yaliyokuwa yanaongozwa na mkufunzi Musa Otieno, nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Harambe stars.