Shirikisho la soka katika eneo bunge la Magarini limethibitisha kuwa ujio wa mashindano ya Omar Mshamu Super Tournament hakutaathiri ligi za fkf katika eneo hilo.
Kulingana na Julius Mweni ambaye ni mwenyekiti wa fkf tawi la eneo hilo amesema kwamba mechi zote za ligi ya fkf zitapewa kipaumbele tofauti na mashindano hayo.
Mweni anasema kwamba kulingana na masharti ya mashindano hayo ni kuwa vilabu vyote vitakavyoshiriki dimba hilo vinafaa kuchukua wachezaji wazawa wa maeneo yao tofauti na wachezaji ambao wamesajiliwa kutoka maeneo mengine kama vile kwenye ligi za fkf.
Mashindano ya Omar Mshamu Super Tournament yataanza rasmi tarehe 26 mwezi Agosti na mechi ya ufunguzi itakuwa ni Super Eagles dhidi ya PAG.