Kucheleweshwa kwa mgao wa fedha za CDF kutoka serikali kuu hadi kwa wabunge mashinani kumelemaza sekta ya michezo kwa miezi mingi jambo ambalo limefanya baadhi ya miradi ya michezo kutofanyika kwa wakati.
Hiyo ni kulingana na mbunge Amina Mnyazi katika hafla ya kupeana vifaa vya michezo mjini malindi kaunti ya kilifi.
Amina Mnyazi amehakikishia wachezaji wa Malindi kufaidika na miradi itakayotumia hela za CDF kupitia ofisi yake.
Wakati hayo yakijiri uongozi wa fkf katika eneo bunge la Malindi umemuomba Amina Mnyazi kuwezesha shirikihso hilo kuandaa mafunzo ya marefa ili kuboresha michezo mashinani.
Kulingana na Dickson Angore ambaye ni afisa wa fkf ni kwamba shirikisho linalenga kuandaa mafunzo ya makocha 30 mwezi November mwaka huu.
