MAKOCHA 29 WAHITIMU KWALE

Huenda Soka la kaunti ya kwale likaimarika hata zaidi baada ya jumla ya wakufunzi  29 wa soka katika eneo la Waa kufuzu hii leo katika kozi ya CAF D diploma chini ya mradi wa SHIFT unaofadhiliwa na kampuni ya basetitanium.

Mohammed Mwachausa ambaye ni mkurugenzi wa shirika la Sambasports youth Agenda amesema kuwa cheti hicho kitawapa nafasi makocha hao kutoa mafunzo ya kandanda katika timu mbalimbali barani Afrika.

Aidha Mwachausa amedokeza kuwa mradi huo wa SHIFT unalenga kukuza talanta za vijana ili waweze kujipatia mapato na kujiepusha na vishawishi potofu kama vile mihadarati na ujambazi.

Kwa upande wake Musa Otieno aliyekuwa msaidizi wa mkufunzi na kapteni wa timu ya kitaifa Harambe Stars ameafiki kuwepo na changamoto za kukuza talanta za kandanda mashinani.

Asha Njama ni kocha wa timu ya Wellers FC aliyefuzu hii leo. Kaunti ya Kwale iko na jumla ya makocha wakike 5.