COASTAL HEROES YAFANYA MAJARIBIO YA WACHEZAJI

Klabu inayoshiriki ligi ya National Super League kutoka ukanda wa pwani Coastal Heroes inajiandaa kufanya majaribio ya wachezaji kama njia moja ya kutafuta talanta za kukiongezea nguvu kikosi hicho kuelekea msimu ujao.

Coastal Heroes yenye makazi yake katika kaunti ya Mombasa inaanza majaribio hayo hii leo kuanzia mwendo wa saa mbili katika uwanja wa Ronald Ngala, majaribio ambayo yataendelea kwa siku tatu.

Msimu uliopita klabu hiyo ilimaliza katika nafasi ya 13 na alama 33 kwenye ligi ya National Super League ambayo ubingwa wake ulikwenda na Shabana FC ambayo ilipanda hadi ligi kuu ya FKF.