Kanisa la Life Ministry Kenya linaendeleza injili ya kumnadi Yesu Kristo kupitia michezo mbalimbali katika kaunti ya Mombasa ambako limekuwa likiandaa michezo ya mara kwa mara na kuwahusisha vijana wa kaunti hiyo.
Akizungumza na Tama la Spoti mapema hii leo Jane Njoki ambaye ni kiongozi wa makanisa yaliyoko chini ya mwavuli wa Life Ministry Kenya ukanda huu wa pwani anazema kwamba wamekuwa wakiazimia kueneza injili miongoni mwa vijana ambao ndio wengi katika jamii.
”Tumeleta pamoja vijana mbalimbali kwenye michezo kuwahubiria baada ya mashindano. Hii ndio fursa ya kuwapata vijana hao kwa sababu michezoni wanapatikana kwa wingi zaidi.” Alisema Njoki.
Njoki ameeleza kuridhika na jinsi ambavyo juhudi za kueneza injili zinazidi kuzaa matunda katika kaunti ya Mombasa huku wakizidisha kampeni hiyo kwa mashirikisho ya michezo mbalimbali.
