UONGOZI WA BULLS UACHIWE JAMII

Meneja wa klabu ya Yanga Fc Collins Omol ndio mdau wa soka wa hivi punde zaidi kutoa kuwa usimamizi wa klabu ya Young Bulls unafaa kupeanwa kwa jamii na wala sio kwa mtu mmoja

Ameyasema hayo baada ya Young Bulls kuzidi kupitia changamoto chungu nzima katika siku ya hivi punde za hivi punde kutokana na kujiondoa kwa Mwenyekiti na mmiliki wa Young Bulls Johnson Mwabati

”Nadhani ingekuwa bora usimamizi uhamie kwa jamii badala ya mtu mmoja kusimamia timu. Pale Mwabati amesaidia hadi sasa nampongeza lakini inafaa sasa wengine waingie na waendelee kuanzia pale.” Alisema Collins

Young Bulls wikendi ilipigwa kichapo cha mabao 5-1 na Bumbani Stars katika uwanja wa Alaskan kwenye mechi ya daraja la kwanza