Naibu wa rasi Profesa Kithure Kindiki amesema kuwa serikali ya Kitaifa inazingatia kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yote ya taifa hili.
Kulingana na Kindiki hakuna wananchi wa maeneo yoyote ya taifa hili watakao baguliwa kwa misingi ya vyama ama mirengo wanayo unga mkono katika taifa hili.
Akihutubia wananchi katika eneo la Nduluku kaunti ya Makueni, Kindiki amewasuta baadhi ya wanasiasa nchini Kenya, kwa kukashifu serikali ya kitaifa huku wakijitafutia uungwaji mkono kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Kindiki amesisitiza haja ya umoja na uuwiano kati ya wananchi wa taifa hili huku akiwataka kujitenga na viongozi wanaopania kuwagawanya kwa misingi ya kikabila na siasa.
…..

