WABUNGE WAENDELEZA VITISHO VYA KUMBANDUA WAZIRI JUSTINE MUTURI MAMLAKANI.

Baadhi ya viongozi wa bunge la kitaifa wamemsuta waziri wa utumishi wa umma nchini Justine Muturi kwa madai ya kuzungumzia masuala ya utekajinyara humu nchini.

Kulingana na viongozi hao wakiongozwa na kinara wa wengi kwenye bunge hilo Kimani Ichungwa na kinara wa wachache Junet Mohammed, wamesema kuwa kauli za Muturi zinachangia kuchipuka wa hisia mseto kati ya ya wananchi dhidi ya serikali ya Kenya kwanza.

Wakizungumza katika kikao cha dharura kwenye bunge hilo, wamesema kuwa iwapo waziri Muturi anahisi serikali anayotumikia inakiuka haki za kibinadam basi anastahili kujiuzulu.

Wawili hao wameibua madai ya kiongozi huyo kujipendekeza kwa wananchi wa taifa hili kutokana na semi ambazo amekuwa akiendeleza kuhusiana na kutekwanyara kwa mwanawe Leslie Muturi.

Aidha viongozi hao sasa wanatishia kumbandua waziri huyo mamlakani kwa madai kuwa amekuwa kuwa na imani na serikali ya Kenya kwanza licha yake kuwa kwenye baraza la mawaziri nchini.