WAHANDISI NCHINI KENYA WATAKIWA KUJISAJILI KWA MAMLAKA YA UJENZI NCA.

Wito umetolewa kwa wahandisi wote nchini kujisajili upya katika mamlaka ya ujenzi nchini NCA (National Contruction Authority), ili kupata muongozo hitajika wa ujenzi katika taifa hili.

Kwa mujibu wa waziri wa ardhi na ujenzi nchini Alice Wahome, mamlaka hiyo sasa imezundua rasmi kanuni hutajika, katika shughuli za ujenzi na kila mhandisi, anapaswa kufuatilia muongozo huo, katika shughuli za ujenzi kote nchini.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, waziri Wahome ametishia kuwa huenda serikali ikawachukulia hatua kali za kisheria, wahandisi ambao watakosa kufuatilia kanuni hizo, kwani wanahatarisha maisha ya wakenya.

Hatua ya kuzinduliwa kwa kanuni hizo, kumechangiwa na ongezeko la idadi ya majumba ambayo, yamekuwa yakiporomoka nchini na kuchangia katika maafa ya wakenya wengi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya bunge la kitaifa kuhusu masuala ya ujenzi wa nyumba, kiongozi ambaye pia mbunge wa Emurua Dikirr, Johana Ngeno ameunga mkono kauli hiyo akisema kuwa, sharti usalama wa wakenya katika masuala ya ujenzi wa majumba nchini uzingatiwe kiukamilifu.