SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI YATUMIA MFUMO WA KILIMO NYUNYIZI KUTATUA TATIZO LA BAA LA NJAA.

Serikali ya kaunti ya kilifi kupitia idara ya kilimo na uchumi wa rasilimali za bahari na maziwa inaendeleza mikakati ya kukabiliana na ukosefu wa chakula jambo ambalo limekuwa likishuhudiwa katika maeneo mbali mbali ya kaunti hii kwa muda mrefu.

Kulingana na  waziri wa kilimo na uchumi wa rasilimali za bahari na maziwa Peterson Chula, idara hiyo imewekeza ekari mia saba katika shughuli za ukulima katika maeneo mbali mbali kaunti hii ya Kilifi.

Chula ametaja hatua hiyo kama njia moja ya kupambana na kosefu wa chakula, unaotokana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayoshuhudiwa kote duniani.

Wakati uo huo, waziri huyo ameeleza kuwa serikali ya  kaunti ya kilifi imetenga fedha katika bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2024/2025, zitakazo piga jegi shughuli za kukabiliana na baa la njaa katika kaunti hii.

Waziri Chula amewahimiza wakaazi wa kaunti ya Kilifi kukumbatia kilimo nyunyizi ili kujikimu kimaisha na hata kuboresha uchumi wa eneo hili.