DROO YA CHAN KUFANYWA LEO

Droo ya mashindano ya mwaka huu ya CHAN inatarajiwa kufanyika rasmi hii leo mwendo wa saa mbili usiku katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi.

Haya yanajiri licha ya jana shirikihso la soka barani Afrika Caf kuthibitisha kuwa mashindano hayo ya CHAN mwaka huu wameahirishwa hadi mwezi Agosti ili kuyapa mataifa andalizi ambayo ni Kenya, Uganda pamoja na Tanzania muda zaidi kukamilisha matayarisho ya mashindano hayo.

Mashindano ya Chan yalikuwa yameratibiwa kufanyika mwezi February kabla ya tangazo hilo kuibuka. Hata hivyo CAF imetangaza kuwa inalenga kutangaza tarehe kamili majuma yajayo.

Kuahirishwa kwa mashindano hayo ni kutokana na maafisa utaalamu wa mashindano ya CAF kushauri shirikisho hilo muda zaidi kutokana na ukosefu wa utayari bayana kwa mataifa haya ya afrika mashariki