UNGANENI MPATE MISAADA YA SERIKALI, FIKIRINI ASHAURI WACHEZAJI

Wito umetolewa kwa vilabu vya michezo mashinani kuungana na kutengeneza vikundi vitakavyosaidia kuanzisha miradi mbali mbali mashinani kama hatua moja ya kukabili ukosefu wa fedha kwa vilabu jambo ambalo linaathiri vilabu vingi kwa sasa.

Fikirini Jacob ambaye ni kiongozi wa vijana alikuwa akizungumza na wachezaji baada ya fainali za mashindano ya talanta soka katika shule ya msingi ya Takaye eneo bunge la Malindi kaunti ya kilifi na amesema kwamba sasa ni wakati wa soka kuimarika kupitia hela za michezo ambazo serikali hutenga kusaidia vijana.

Fikirini amewashauri kuungana katika vikundi vitakavyosaidia kupata cheti ambacho kitawawezesha kuitisha misaada kwa serikali za mashinani ili kukuza talanta za vijana wengi pamoja na ajira.