MUYEYE ALLSTARS NDIO MABINGWA WA TALANTA SOCCER PROJECT

Muyeye Allstars ndio mabingwa wa makala ya tano ya Talanta Soccer Project mashindano yaliyofanyika na kutamatika katika kaunti ya kilifi.

Muyeye Allstars walichukua ubingwa huo baada ya kuitandika klabu ya Bayern Ngalla kupitia ufundi wa upigaji wa matuta baada ya dakika 90 kutamatika sare tasa katika uwanja wa shule ya msingi ya Takaye.

Akizungumza na Tama la Spoti Sifa Kahindi ambaye ni Nahodha wa kikosi cha mabingwa Muyeye Allstars amesema ipo haja ya viongozi kushika mkono vilabu vya mashindani katika juhudi za kutimiza ndoto zao kama wachezaji.

Muyeye Allstars itakuwa  inashiriki ligi ya kaunti ya Kilifi kwa msimu wa tatu mfululizo sasa, msimu wa mwaka 2023/2024 unaotarajiwa kuanza rasmi mwezi February mwaka huu.