BUNGE LA KILIFI KUUNDA TIMU YA KAUNTI

Bunge la kaunti ya Kilifi linalenga kutengeneza kikosi cha soka kitakachowakilisha kaunti nzima ya kilifi. Kikosi hicho kitachojumuisha wachezaji kutoka maeneo mbali mbali ya kaunti hii.

Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wadi mteule wa bunge la kaunti ya Kilifi Betty Kache wakati akizungumza na wachezaji walioshiriki katika mashindano ya Talanta Soka katika uwanja wa shule ya msingi ya Takaye eneo bunge la Malindi Kaunti ya Kilifi.

Kulingana na Betty Kache ni kuwa mpango huo unalenga kunufaisha vijana hasa wale  watakaopata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho kwenye kuinua na kukuza vipawa vyao pamoja na kujipatia ajira.