KISUMU ALLSTARS YALIA ‘NJAA’

Klabu ya Kisumu Allstars inaomba wahisani kuwapiga jeki kuheshimu ratiba ya mechi yao ya wikendi.

Mkurugenzi mkuu wa kikosi hicho Nicholaus Ochieng anahofia huenda wakakosa kucheza mechi yao ya kesho dhidi ya Mombasa Elites katika dimba la Mbaraki.

Klabu hiyo tangu mwezi September mwaka jana haijalipa mishahara kwa benchi la kiufundi pamoja na kutokana na ukosefu wa fedha jambo ambalo kwa sasa linakatisha tama wachezaji.