UHISPANIA NDIO MABINGWA EURO

Uhispania ndio mabingwa wa mashindano ya Euro yalokuwa yanaendelea nchini Ujerumani baada ya usiku wa kuamkia leo kusajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza.

Bao la Nico Williams kunako dakika ya 47 na lile la Mikel Oyarzabar anayechezea Real Sociodad kama kiungo ndio mabao yaliyotosha kuishindia uhispania inayofunzwa na kocha Luis De la fuente uingwa wao wa nne wa mashindano haya.

Bao la kufutia machozi kwa Uingereza limefungwa na Cole Palmer anayechezea Chelsea ambaye usiku wa leo ameingia kama mchezaji wa akiba.

Mchezaji bora katika mashindano ya Euro msimu huu tuzo hio amepewa kiungo Rodri anayechezea uhipania pamoja na Manchester City.

Mchezaji bora mchanga katika mashondano haya ni Lamine Yamal mchezaji wa Barcelona mwenye umri wa miaka 17.