SILVER BULLETS BAADA YA KUACHANA NA KOCHA WAO SASA YASHUKA DARAJA

Klabu ya Silver Bullets haitashiriki ligi ya Fkf daraja la pili kitaifa msimu ujao baada ya kushushwa daraja.

Klabu hiyo yenye makazi yake Vipingo katika kaunti ya Kilifi ilikosa kusafiri na kushiriki mechi tatu za ligi na kwa mujibu wa sheria tayari imeshuka daraja kwa hilo.

Hayo yanajiri majuma machache baada ya kocha mkuu wa klabu hiyo Sammy Karisa kujiuzulu kwa kile alichokitaja kuwa kukosa ushirikiano baina yake na viongozi wengine, wachezaji na hata mashabiki kuhusu upangaji wa kikosi cha kwanza.

Silver Bullets sasa inakwenda kufanana na Ashton Rangers kutoka kaunti ya Mombasa ambayo pia imeshashuka daraja kutokana na kukosa kuheshimu Ratiba mara tatu.