TAARIFA ZA SOKA ULAYA ; MBAPPE KUTANGAZWA MADRID, SOUTHGATE KUJIUZULU, MULLER NA SHAKIRI KUSTAAFU

Mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate amejiuzulu kutoka wadhifa wake hii leo.Hii ni baada ya kupoteza fainali ya pili ya Euro ambako Uingereza (Three Lions) walipigwa kichapo cha mabao 2-1 na Uhispania. Hii ni fainali ya pili mfululizo Uingereza inapoteza chini ya Southgate baada ya kupoteza makala yalopita dhidi ya Italia katika matuta.

Kylian Mbappe ametamgazwa rasmi leo kuwa mchezaji wa klabu ya Real Madrid katika Dimba la Santiago Barnebou. Mbappe alisajiliwa kwa uhamisho huru kutoka PSG majira haya ya kiangazi na kilichokuwa kinasubiriwa ni kutamatika kwa Mashindano ya Euro ili atangazwe rasmi leo.

Katika hafla iliyoongozwa na rais wa Real Madrid Florentino Perez Mbappe ametangaza kuwa analenga kujituma na kuihudumia klabu yake mpya kwa hali na mali. Mbappe amepewa jezi nambari tisa mgogoni jezi ambayo inakumbukwa kuvaliwa na miamba kama vile Raul lakini pia siku za hivi punde Karim Benzema.

Kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani Thomas Muller amefangaza rasmi hii leo kuwa amestafu soka la kimataifa. Ameyasema hayo baada ya mashindano ya Euro ambayo Ujerumani walikuwa wenyeji.

Katika uchezaji wake wa soka la kimataifa Muller amefunga mabao 45 katika mechi 131 ambazo ameshiriki, katika kipindi chake amejishindia kombe moja la dunia.

Mwengine ambaye amestafu soka la kimataifa Xherdan Shaqiri ambaye amechezea timu yake ya taifa la Uswizi mechi 125