MASHINDANO YA DOLA SUPER CUP KUANZA KILIFI

Mashindano ya Dola Super Cup yanatarajiwa kuanza rasmi katika kaunti ya kilifi katika kipindi cha takriban wiki moja ijayo na mechi ya kwzanza itachezwa katika uwanja wa chuo kikuu cha Pwani mjini kilifi.

Kulingana na waandalizi wa mashindano hayo ni kuwa yanalenga kuvumbua talanta ambazo zitaangaziwa kwenda mbele huku maskauti wa timu mbalimbali ikiwemo klabu ya Bandari kutoka Mombasa klabu ya ligi kuu ya fkfk hapa nchini Kenya ikitarajiwa kuwa mashinani kuangazia talanta hizo.

Athman Ali Said ambaye ni kati ya wasimamizi wa mashindano hayo anasema timu zinatoka katika kila maeneo bunge ya kaunti ya Kilifi.

Ali Said anasema wameshirikiana na makoch wa mashinani kwenyekutafuta wachezaji ambao sasa wameunda timu zitakazoshiriki mashindano hayo makala ya kwanza kabisa katika kaunti ya kilifi baada ya kuendelea katika kaunti nyingine kama vile Kwale na Mombasa.