Shule ya upili ya Malindi High imeanza mikakati ya kurudisha hadhi ya mchezo wa raga katika eneo bunge la Malindi kupitia makuzi ya talanta kutoka umri mchanga, zoezi zinalofanywa na makocha lakini pia walimu wa michezo.
Akizungumza na Tama La Spoti Kenedy Kirinywa mwalimu na kocha anayesimamia michezo katika shule hiyo ni kuwa raga sasa imeanza kufundishwa kwa wanafunzi kutoka kidato cha kwanza ili kuanza kuzoea mchezo huo na kuaanza kuunda kikosi bora cha shule.
Kirinywa pia amewahimiza wachezaji wachanga wanaojifunza raga kuzingatia sana nidhamu iwapo wangependa kukua bora katika mchezo huo siku za usoni. Amekanusha mtazamo wa wengi wa wanafunzi lakini pia wazazi ambao huwakataza watoto wao kucheza raga kisa ni mchezo hatari.
Shule ya upili ya Malindi High ndio mabingwa wa raga za wachezaji saba kila upande katika mkoa huu wa pwani na wamejikatia tikiti kushiriki mashindano ya kitaifa yatakayoandaliwa kaunti ya Kisii.

