TAARIFA ZA UHAMISHO ULAYA ; MODRID, ALVAREZ, INACIO

Luka Modric mchezaji wa timu ya taifa ya Croatia sasa amechaguliwa kuwa nahodha mpya wa klabu ya Real Madrid inayoongozwa na Carlo Ancelotti

Hii ni baada ya aliyekuwa nahodha wa klabu hiyo Nacho Hernandes kukamilisha uhamisho wake kuelekea Saudi Arabia Pro League.

Hayo yanajiri baada ya Modric pia kurefusha mkataba wake wa mwaka mmoja na klabu yake Madrid ambao utatamatika mwishoni mwa mwezi Juni 2025.

Klabu ya Manchester City inalenga kufanya mazungumzo na mchezaji wao wa kimataifa wa Argentina Julian Alvarez, 24, baada ya fainali za mashindano ya  Copa America. Klabu ya Paris St-Germain inavutiwa na mshambuliaji huyo, ambaye anataka muda zaidi wa kucheza, lakini City wanataka kusalia naye.

Klabu ya Liverpool wamemweka mlinzi wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Goncalo Inacio, 22, kuwa mlengwa wao mkuu katika kipindi cha uhamisho. Hii huenda ikawa sajili ya kwanza ya kocha mpya wa klabu hiyo Arne Slot ambaye analenga kujenga kikosi kipya.