Naibu kocha mkuu wa timu ya taifa ya Harambee Stars Ken Odhiambo ametangazwa kuwa kucha mkuu wa klabu ya Bandari Fc kutoka kaunti ya Mombasa kuelekea msimu wa mwaka 2024/2025.
Odhiambo sasa anatarajiwa kusadia na mkufunzi John Baraza kwenye kuinoa klabu hiyo ya Pwani ambayo inalenga kuwinda ubingwa wa ligi ya FKF Msimu ujao.
Ujio wa Odhiambo umemaliza tetesi zote za kuhusisha Bandari na kocha wa zamani wa Tusker Fc Robert Matano mashabiki wengi wakizungumza awali kuwa kipindi hiki ambacho Bandari ilikuwainatafuta kocha, Matano angefaa sana kuiongoza klabu hiyo ya Mbaraki.
Kwa sasa Robert Matano ni kocha ambaye hana klabu na hakujakuwa na taarifa zinazomhusisha na klabu nyingine baada ya kuachana na Wanamvinyo mkataba wake ulipotamatika mwishoni mwa mwezi juni.

