HARAMBEE STARS YASALIA NAFASI 108 FIFA, ARGENTINA IKISHIKA KILELE KWENYE VIWANGO VIPYA

Timu ya taifa ya Kenya Harambe Stars imesalia katika nafasi yake ya 108 katika viwango vipya vya fifa vilivyotolewa hivi punde. Majirani Uganda wako mbele ya Kenya huku duniani kwenye viwango hivyo wakisiamama katika nafasi ya 95 huku Tanzania ikiwa chini ya Kenya na iko katika nafasi ya 113.

Duniani timu ambayo kwa sasa iko nafasi ya kwanza kwenye viwango vya soka ni Argentina ambao ni mabingwa wa mashindano ya kombe la dunia 2022 pamoja na kutetea ubingwa wao wa kopa America mwaka huuu.

Ufaransa iko nafasi ya pili huku timu ya taifa ya Uhispania ikipanda nafasi tano na kufika katika nafasi ya tatu ulimwenguni. Hii ni baada ya kampeni yao nzuri na yenye mafanikio katika mashindano ya Euro 2024.

Mashindano ya kimataifa ya Euro, Copa America, Afcon pamoja na yale ya vilabu vya kimataifa ndio chanzo kikubwa ambacho kimechangia takwimu hizi kufanyika na viwango vipya kupatikana.