Mashindano ya dola super ambayo yameendelea katika kaunti za mkoa wa pwani wiki ijayo yataingia katika kaunti ya kilifi na yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 27 mwezi July.
Kulingana na waandalizi wa mashindano hayo mwisho wa kwisha mshindi atajishindia shilingi milioni moja.
Kulingana na Saddam Suleiman ambaye ni meneja wa mauzo katika kampuni ya Dola ni kuwa Kilifi mashindano hayo ya soka yatahusisha timu nane za wavulana huku bingwa akisafiri kwa ajili ya mashindano ya kimkoa katika kaunti ya Mombasa ambako sasa bingwa atakuwa anatuzwa.
Suleiman amethibitishakuwa kwa sasa mashindano haya yanahusisha timu za wavulana peke yake. Amewaomba mashabiki kujitokeza ili kushabikia timu zao huku tamati ya mashindano haya kunatarajiwa kuwa na zawadi chungu nzima kwa wachezaji bora katika kila kitengo lakini pia timu bora sawa na mashabiki

