ARGENTINA WATETEA UBINGWA COPA AMERICA

Argentina ndio mabingwa wa fainali za Copa America mashindano yalokuwa yanaendelea katika taifa la Marekani. Argentina ambao ni mabingwa watetezi wameichapa Colombia kichapo cha bao 1-0, bao la Lautaro Martinez anayechezea Inter Milan ndio bao lilotosha kuipa ubingwa tena Argentina inayoongozwa na mkufunzi Leonel Scaloni.

Fainali hiyo imetamatika mwendo wa saa moja asubui hii baada ya kucheleweshwa kuanza mwendo wa saa tisa. Taarifa zinasema mechi hiyo imelazimika kuanza saa 4.15 kutokana na vurugu lililotokea uwanjani pale mashabiki ambao hawakuwa na tiketi wamelazimisha kuingia kwenda kuona fainali hiyo.

Hata hivyo baada ya maafisa wa kiusalama kudhibiti hali hiyo ya vurugu mechi ikaanza lakini ikalazimika kuingia katika dakika 30 za muda wa ziada baada ya zile 90 kuisha ikiwa sare tasa.

Lautaro Martinez ameifungia argentina bao la ushindi katika dakika ya 112 na kuipa Argetina ubingwa wao wa 16 katika historia.