Wachezaji sita wa mashindano ya Euro wameibuka washindi wa kiatu cha dhahabu katika makala ya Ujerumani mwaka huu.
Sita hao wote walifunga mabao matatu na ni pamoja na Harry Kane wa Uingereza, Dani Olmo wa Uhispania, Cody Gakpo wa Uholanzi, George’s Mikautadze wa Georgia, Jamal Musiala wa Ujerumani pamoja na Ivan Schranz wa Slovakia.
Kiungo wa Manchester City na Uhispania Rodri ndio mchezaji bora wa Euro 2024 huku Lamine Yamal raia wa Uhispania mwenye umri wa miaka 17 ndiye mchezaji bora chipukizi katika mashindano hayo ambayo Uhispania waliibuka mabingwa kwenye ushindi wa 2-1 usiku wa kuamkia leo.

