UHAMISHO WA DARAJA LA PILI WAPAMBA MOTO

Mohamed Ramadhan ambaye amekaa nje sasa kutokana na kukosa klabu sasa ni rasmi kuwa amepata hifadhi katika klabu ya Inter Dabaso inayoshiriki ligi ya daraja la pili kitaifa.

kulingana na mkufunzi Sammy wa klabu ya Inter Dabaso ni kwamba kila kitu kishwari kwa Rama kujiunga na klabu hiyo yenye makazi yake mjini watamu, kaunti ya Kilifi.

Kelvin Charo maarufu kama ‘Maestro’ sasa amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu yake mpya ya Omax akitokea klabu ya Yanga.

Maestro anatarajiwa kucheza mechi ya kwanza kabisa katika uwanja wa shule ya wasichana ya Joho Girls siku ya jumapili watakapokuwa wanashuka dimbani na klabu ya Kishada.

Kelly Maestro amesema analenga kuisaidia klabu yake mpya kusajili matokeo mazuri msimu pamoja na kuipandisha daraja hadi daraja la kwanza kitaifa.