Wanamvinyo Tusker wanaoongozwa na mkufunzi Robert Matano sasa wameanza kufufua matumaini yao ya kutetea ubingwa wa fkf kwa kusajili ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bidco United mchana wa leo.
Kwa sasa Tusker inasimama katika nafasi ya pili wakiwa na alama 39 wakiwa na mechi moja kiporo huku Gor Mahia wakiongoza ligi na alama 45.
Gor Mahia kwa upane wao wameirangaranga Vihiga Bullets kichapo cha mabao 5- 0,
Kariobangi Sharks wamepiga sare ya mabao 2-2 dhidi ya klabu ya Wazito fc.
Matokeo mengine;
Nairobi City vs Mathare United 3-0
AFC Leopards vs Bandari 1-0
Kakamega Homeboys vs KCB 0-0

