Mkufunzi Engin Firat amesema kwamba amefurahishwa na matokeo yajana ya vijana wake wake Harambee Stars licha ya kwamba walipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya timu ya taifa ya Iran.
Mkufunzi huyo amesema kwamba vijana wake walionyesha mchezo mzuri licha ya kwamba wamekaa muda mrefu nje ya soka la kimataifa.
Mkufunzi huyo amesistiza kwamba vijana wake sasa wanahitaji muda zaidi kushikana miguu ili kuleta umoja kimchezo katika mashindano yajayo na kusema kwamba mechi ya jana ilikuwa sahihi kujipima kiwango chao.

