UHAMISHO, MAESTRO AJIUNGA NA OMAX FC

Kiungo wa kati wa klabu ya Kipaji Tezo Emmanuel Haro sasa amehamia klabu ya daraja la pili kitaifa Furunzi fc. Uhamisho huo umethibitishwa rasmi na meneja wa timu hiyo Nyale Suntkay kwamba sasa Haro atakuwa mchezaji wa Furunzi FC kwa muda ambao bado haujabainika.

Kwengine ni kwamba Kelly Maestro kiungo wa Yanga klabu inayotokea mji wa Malindi Kaunti ya Kilifi amehamia klabu ya Omax fc inayoongozwa na mkufunzi Juma Kalato.

Maestro ameachana na klabu ya Yanga kwa makubaliano yaliyoafikiwa na pande zote mbili. Maestro ni mchezaji ambaye amekipiga katika klabu ya Samburu Lions lakini pia Malindi Progressive kabla ya kuhamia Yanga na hatimaye sasa Omax fc.